Baridi yauwa watu 25 Poland.
Watu wasiopungua 25 wameuawa mwishoni mwa wiki nchini Poland kutokana na baridi kali, wakati wa moja ya majira ya baridi zaidi nchini humo. Polisi imewatolea mwito raia kuwa macho kutambua yeyote anaekabiliwa na hatari ya kushuka kwa viwango vya joto mwilini, hasa watu wasio na makaazi, walevi au wazee. Watu 14 wameripotiwa pia kufariki katika milima ya Tatra, iliyoko kati ya Poland na Slovakia. Majira ya baridi ya Poland yamechelewa kuwasili safari hii, kama ilivyokuwa kwa kipindi kilichopita, wakati watu 77 walipofariki kutoana na baridi kali.
No comments:
Post a Comment