Mwanamuziki David Bowie aaga dunia
Mwimbaji maarufu David Bowie, ameaga dunia akiwa na umri miaka 69, baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani.
Mwanawe Duncan Jones amethibitisha kifo chake na kutoa taarifa rasmi katika mitandao yake ya kijamii.
Taarifa hiyo ilisema kuwa David Bowie alifariki nyumbani kwake, akiwa na familia yake.
Taarifa hiyo imeelezea kuwa Bowi amekuwa akiuguza ugonjwa huo kwa muda wa miezi kumi na minane.
Aidha ametoa wito kwa mashambiki wake kuwapa muda wa kuomboleza kifo chake.
Bowie alifanya tamasha yake ya mwisho mwaka wa 2006, mjini New York kuchangisha pesa za kutoa misaada ya kibinadamu.
Blackstar, ambayo inajumuisha nyimbo saba, imepata umaarufu mkubwa.
Bowie alipata sifa chungu nzima mwaka wa 1972 wakati aliposhirikishwa katika filamu mbili za The rise and Fall of Ziggy Stardust na ile ya Spiders from Mars.
Miongoni mwa nyimbo alizoimba ni pamoja na Let's Dance, Space Odditty, Heroes, Under Pressure, Rebel Life on Mars na Suffragette City.
Bowie alizaliwa mjini London na kupewa jina David Jones Januari 8, 1947, lakini mwaka wa 1966 akabadili jina wakati alipopata umaarufu mkubwa.
Alijiunga na bendi kadhaa kabla ya kupata mkataba na kampuni ya kunakili muziki ya Mercury Records, iliyotoa albamu zake za Man of Word, Man of Music mwaka wa 1969 iliyojumuisha wimbo wa Space Odditty ambao ulikuwa maarufu sana nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment