Sunday, January 3, 2016


Gavana wa jimbo moja katikati mwa Mexico, ameiagiza kamisheni ya usalama wa jimbo kuchukuwa uongozi wa polisi katika miji kadhaa, baada ya meya kuuawa, katika uhalifu ulioelezwa kama kitisho cha genge la wahalifu kwa mameya wengine. Gavana Graco Ramirez ameiagiza kamisheni hiyo kuchukuwa majukumu katika manispaa 15 katika jimbo la Morelos, ikiwemo na mji mkuu wa jimbo hilo Cuernavaca, na Temixco, ambako meya alieuawa alikuwa akihudumu. Meya huyo Gisela Mota mwenye umri wa miaka 33, alipigwa risasi na kuuawa siku ya Jumamosi, zikiwa karibu saa 24 tangu alipokula kiapo cha kuongoza mji huo wa Temixco, ulioko umbali wa kilomita 90 kusini mwa mji mkuu wa Mexico, Mexico City. Ramirez amewambia waandishi habari kuwa mauaji ya meya Mota, ni ujumbe na kitisho cha wazi kwa mameya wengine waliochaguliwa hivi karibuni, kutokubali mfumo wa uratibu wa polisi unaolenga kulisafisha jeshi hilo linalolalamikiwa kushirikiana na wahalifu

No comments:

Post a Comment