Thursday, January 7, 2016

Image result for Iran, Saudi
Mzozo wa kidiplomasia kati ya Saudi Arabia na Iran unazidi kufukuta, huku Iran ikiitaka Saudi Arabia kuachana na msimamo wake wa mkabiliano. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, ameitaka Saudi Arabia kuacha kuchochea wasiwasi na kujibu hatua zake za karibuni, ambazo zilisababisha mkwamo huo. Iraq imemtuma waziri wake wa mambo ya nje nchini Iran na pendekezo la kuwa mpatanishi kati ya madola hayo makuu ya kanda ya mashariki ya kati, ikihofia kuwa mripuko mpya wa vurugu za kiitikadi unaweza kuhatarisha kampeni yake dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu. Mzozo kati ya Iran na Saudi Arabia ulianza siku ya Jumamosi, baada ya Saudi kuwauwa watu 47, akiwemo kiongozi maarufu wa Kishia. Waandamanaji nchini Iran wakauchoma moto ubalozi wa Saudi Arabia pamoja na ubalozi wake mdogo mjini Mashhad.

No comments:

Post a Comment