Monday, January 11, 2016

Image result for Cologne

Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la North-Rhine Westphalia, Ralph Jäger, amesema sehemu kubwa ya watu wanaoshukiwa kufanya mashambulizi ya kingono katika Mkesha wa Mwaka Mpya walikuwa ni wageni. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Jäger amesema baadhi ya washukiwa hao ni wale waliongia Ujerumani kuomba hifadhi ya ukimbizi kutokea nchi zenye migogoro, ikiwemo Syria.
Wakati huo huo, polisi nchini Ujerumani imesema kundi la wageni kutoka Pakistan na Syria limeshambuliwa mjini Cologne. Duru za polisi zimeeleza kuwa Wapakistan sita walivamiwa na kundi la watu takribani 20 hapo jana, na kwamba wawili miongoni mwao walilazimika kulazwa hospitalini kwa muda.
Siku hiyo hiyo raia wa Syria alishambuliwa na kujeruhiwa na watu 5, lakini hakuhitaji matibabu. Polisi imesema bado inachunguza iwapo mashambulizi hayo yalifanywa kwa misingi ya kibaguzi, na kama yanahusiana na matukio ya Mkesha wa Mwaka Mpya.

No comments:

Post a Comment