Mjadala wa televisheni bila ya Trump.
Mgombea mmojawapo wa kiti cha rais kutoka chama cha Republican nchini Marekani,Donald Trump ametekeleza aliyoyasema na hakushiriki katika mjadala wa televisheni wa wagombea wa chama hicho kabla ya zoezi la kwanza la kumchagua mgombea wa chama hicho. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Fox News,kilichoandaa mjadala huo,Trump alitaka alipwe dala milioni 5 ili kushiriki katika mjadala huo. Alitaka fedha hizo zitiwe katika fuko la wakfu wake. Kituo cha Fox News kimeyakataa madai hayo. Badala ya kushiriki katika mjadala wa televisheni,tajiri huyo mwenye kumiliki majumba alikwenda Moines-mji mkuu wa jimbo la Iowa kukusanya fedha kwa ajili ya wapiganaji wa zamani wa vita. Zoezi la kwanza la kumchagua mgombea wa chama cha Republican katika jimbo la Iowa litafanyika Jumatatu ijayo. Donald Trump anaongoza matokeo ya kura ya maoni ya wananchi kwa upande wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment