Baraza la mawaziri lajadili kuhusu kutumwa wanajeshi wa ujerumani Mali na Iraq.
Baraza la mawaziri la serikali kuu ya Ujerumani linaamua hii leo kuhusu kuzidishwa idadi ya wanajeshi nchini Mali na kaskazini mwa Iraq. Ujerumani inapanga kutuma wanajeshi hadi 650 kutumikia kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali. Watasaidia miongoni mwa mengineyo kuhakikisha makubaliano ya amani yanaheshimiwa. Kinyume na hali namna ilivyokuwa miezi iliyopita, wanajeshi wa Ujerumani watawekwa zaidi safari hii katika maeneo hatari ya kaskazini mwa Mali. Zaidi ya hayo serikali kuu ya Ujerumani inapanga kuzidisha idadi ya wanajeshi wanaotoa mafunzo kaskazini mwa Iraq. Wanajeshi hadi 150 wa Ujerumani - Bundeswehr, watawapatia mafunzo wanamgambo wa kikurd Peshmerga wanaopambana na wafuasi wa itikadi kali wa Dola la Kiislam - IS. Hadi wakati huu wanajeshi 100 tu wa Ujerumani ndio waliokuwa wakiruhusiwa kushiriki katika zoezi kama hilo.
No comments:
Post a Comment