Rais wa Guatemala aapishwa.
Jimy Morales ambaye ni mwigizaji mchekeshaji wa zamani katika Televisheni ameapishwa rasimi hapo jana kuwa Rais wa Guatemala katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa miongoni mwao kutoka katika mataifa ya Marekani, Mexico na Ecuador. Uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana ulimuwezesha Morales kupata ushindi mkubwa licha ya kutokuwa na uzoefu mkubwa wa kisiasa. Alipata ushindi huo katika kipindi ambacho wananchi wa taifa hilo walikuwa wakilalamikia kukithiri kwa vitendo vya rushwa chini ya utawala wa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Otto Perez. Baraza lake la mawaziri lilikuwa likitatarajiwa kutangazwa saa chache baada ya tukio la kuapishwa kwake. Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden ni miongoni mwa walioudhuria hafla hiyo ambaye alimpongeza Morales kwa azima yake ya kupambana na vitendo vya rushwa katika taifa hilo lenye watu milioni 16.
No comments:
Post a Comment