Poland waandamana kupinga mabadiliko ya uhuru wa vyombo vya habari.
Maelfu ya wapinzani wa serikali mpya ya Poland ya mrengo wa kulia, wanaojiita Kamati ya Ulinzi wa Demokrasia, waliandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Warsaw pamoja na miji mengine jana dhidi ya sera wanazosema kuwa zinahatarisha demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini humo. Waandamanaji hao wanasema mabadiliko ambayo serikali imeyafanya ya kuiweka mahakama ya katiba pamoja na vyombo vya habari vya serikali chini ya udhibiti wa chama tawala cha Law and Justice, yanatishia uhuru wa vyombo vya habari pamoja na Demokrasia ya nchi. Hatua hizo pia zimewashitua baadhi ya viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya, na Halmashauri ya Umoja wa Ulaya itajadili utawala wa sheria katika nchi hiyo hapo Jumatano.
No comments:
Post a Comment