Sunday, January 10, 2016


Image result for MAHARAMIA WA KISOMALI
Takriban wahamiaji 12 wa asili ya Kisomalia na Kiethiopia wamefariki ndani ya boti iliyopotea njia kwa kuchukuliwa na maji ikiwa inaelekea nchini Yemen. Walinzi wa pwani waliiokoa boti hiyo Ijumaa, ambayo ilikuwa imechukuliwa na maji kwa siku kadhaa kutokana na matatizo ya kiufundi. Maiti 12 zimegunduliwa ndani ya boti hiyo, pamoja na watu wengine 70 waliokuwa katika hali mbaya kutokana na njaa na kukosa maji mwilini. Wengi wa wahamiaji hao, waliopanda boti hiyo katika bandari ya Bosaso nchini Somalia, wanaaminiwa kuwa ni Waethiopia.

No comments:

Post a Comment