Thursday, January 7, 2016


Image result for libyan people
Bomu lililokuwa limetegwa katika gari hii leo limeripuka katika kambi moja ya mafunzo ya jeshi la polisi nchini Libya na kuwaua askari polisi 60 n kuwajeruhi wengine 200. Shambulizi hilo lilifanyika katika lango kuu la kambi hiyo katika mji wa pwani wa Zliten ulioko kilometa 160  Mashariki mwa mji mkuu, Tripoli. Hakukuwa na taarifa za watu waliohusika na shambulizi hilo.  Libya imekuwa ikiandamwa na mashambulizi tangu kuondolewa madarakani kwa Muammar Gaddafi mwaka 2011. Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta pia limegawanyika katika pande mbili za kisiasa za bunge zinazohasimiana na ambazo kila mmoja unaungwa mkono na makundi tofauti ya wanamgambo. Kundi la itikadi kali la Dola la Kiislamu IS imekuwa likitumia mwanya wa tofauti hizo za kisiasa kujiimarisha nchini humo. Mwezi uliopita makundi hayo mawili ya kisiasa yalisaini makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ingawa baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi mkubwa wamekuwa wakiipinga hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment