Jaribio la nyuklia la Korea ya Kaskazini lakosolewa.
Korea ya Kaskazini inasema imefanikiwa kufanya jaribio la bomu la atomiki, ambalo ni hatua moja kubwa kueleka bomu kamili la nyuklia. Habari hizo zimetangazwa na msemaji wa serikali kupitia televisheni ya nchi hiyo. Marekani, Korea ya Kusini na Japan zimelaani kitendo hicho. Katika jamhuri ya umma wa China, shirika rasmi la habari Xinhua limesema jaribio hilo linajongelea lengo la kutengeneza bomu la kinyuklia. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura leo kuzungumzia suala hilo. Hata hivyo, Marekani inashuku kama maelezo yaliyotolewa na Pyongayang ni sahihi. Msemaji wa baraza la usalama wa taifa amesema mjini Washington, kwa sasa hawawezi kuthibitisha habari hizo. Nchi hiyo ya kikominusti iliyotengwa na jumuia ya kimataifa imeshawahi kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia mwaka 2006, 2009 na 2013 na kukabiliana kila wakati na laana za walimwengu. Na kila jaribio la nyuklia hupelekea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo zaidi serikali ya Pyonyang.
No comments:
Post a Comment