Wednesday, January 6, 2016

Kwa mujibu wa ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Marekani, wanamgambo wa itikadi kali wa Dola la Kiislam, IS, wamepoteza takriban asilimia 30 ya maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti nchini Syria na Iraq. Msemaji wa ushirika huo amesema mjini Baghdad asili mia 40 ya ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na IS imekombelewa na nchini Syria ni asili mia 20. Wanamgambo wa itikadi kali walinyakua sehemu kubwa ya ardhi ya nchi hizo mbili mwaka 2014. Nchi shirika zinazoongozwa na Marekani zinapambana kwa njia ya angani dhidi ya IS nchini Syria na Iraq. Kaskazini mwa Iraq, wanamgambo wa Kikurdi - Peshmerga - wanapigana na IS na katika sehemu nyengine za nchi hiyo, wanajeshi wa Iraq na wanamgambo wa Kishia wanapigana dhidi ya IS. Nchini Syria, Urusi pia imeanzisha mashamabulio ya angani dhidi ya IS tangu mwishoni mwa mwezi wa Septemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment