Thursday, January 7, 2016

Ikulu ya Marekani White House jana imekanusha madai ya Korea Kaskazini kwamba ilifanya jaribio lililofanikiwa la bomu la nyuklia kwa mara ya kwanza. Msemaji wa White House Josh Earnest, amesema uchambuzi wa awali unakinzana na madai ya Korea Kaskazini, na kuongeza kuwa hakuna kitu kama hicho kilichotokea katika muda wa saa 24. Madai ya Korea Kaskazini yalitolewa kupitia televisheni ya taifa mjini Pyongyang, ambayo ilitangaza kuwa jaribio la kwanza la bomu la nyuklia la Jamhuri lilifanyika kwa mafanikio majira ya saa nne asubihi. Rais Barack Obama amezungumza kwa njia ya simu na rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye na kumhakikishia dhamira ya Marekani kwa usalama wa taifa hilo. Rais Obama pia amezungumza na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe. Barazala la usalama la Umoja wa Mataifa limesema linatafakari vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini, ambayo imefanya majaribio matatu ya nyuklia tangu mwaka 2006, ikikaidi maazimio ya Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment