Friday, February 26, 2016
Alshabab wadai kufanya shambulizi katika hoteli moja mjni Mogadishu.
Kiasi ya watu zaidi ya tisa wakiwemo raia wameripotiwa kuuawa nchini Somalia katika tukio lililohusisha mashambulizi ya risasi kati ya watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Al- Shabab na walinzi wa hoteli moja iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo , Mogadishu kabla ya vikosi vya usalama vya serikali kuingilia kati na kuzima shambulio hilo. Duru kutoka nchini humo zinaarifu kuwa kiasi ya wanamgambo watano waliuawa huku pia raia tisa wakidaiwa kuuawa katika tukio hilo. Mtu mmoja aliyekuwa amebeba miripuko katika gari alijiripua kwa kujitoa muhanga baada ya kuliingiza gari hilo kwa nguvu katika lango la hoteli hiyo ijulikanayo kama SYL hapo jana usiku na kutoa mwanya kwa watu waliokuwa na bunduki kutumia fursa hiyo kujaribu kulazimisha kupita katika kizuizi cha kwanza cha ulinzi ingawa washambuliaji hao hawakufanikiwa kupita katika kizuizi cha pili cha lango la hoteli hiyo. Washambuliaji wanne waliokuwa na bunduki pamoja na mtu aliyejitoa muhanga ni miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo. Kundi la Al- Shababu limedai kuhusika na shambulizi hilo.
Mwigizaji wa filamu ya Rocky Tony Burton afariki.
Tony Burton aliyeshiriki katika filamu sita za Rocky dhidi ya Sylvester Stallone amefariki akiwa na umri wa miaka 78.
Kiini cha kifo chake bado hakijulikani ,lakini dadaake ,Loretta Kelly amesema kuwa amekuwa akienda hospitalini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Ameongozea kuwa hajapata utambuzi wa ugonjwa wake katika wakati huo na kwamba hali yake ya afya ilikuwa imezorota hali ya kutoweza kuiona filamu ya Creed.
Uigizaji wake ulimsaidia Creed ambaye ni mpinzani wa Rocky Balboa katika filamu mbili za kwanza za masumbwi kabla ya kuwa mkufunzi wa Balboa.
TCU YAHAMIA ARUSHA NA SAKATA LA KUVIFUTIA VIBALI VYUO VISIVYO KIDHI.
February 26 2016 taarifa kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)ilikuwa ni hii ya kukifutia kibali Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT), kampasi ya Arusha na kuwahamisha wanafunzi wote waliokuwa wanasoma katika kampasi hiyo kwa gharama za Chuo hicho.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini Prof. Yunus Mgaya amesema ‘Kwa muda mrefu na kwa wakati tofauti kumekuwapo na matukio ya migogoro baina ya uongozi wa Chuo na Wanafunzi, Kwa kipindi hicho chote tumekuwa tukifuatilia kwa ukaribu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki‘
Gianni Infantino ndio rais mpya wa Fifa.
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.
katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.
Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini mshindi wa moja kwa moja.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa''.
Wednesday, February 24, 2016
Uchumi wa Afrika Kusini uko 'taabani'
Uchumi wa taifa la Afrika Kusini uko katika hali mbaya,waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan amesema.
Tamko hilo lilijiri kabla ya hotuba yake ya matumizi ya serikali ambapo alipunguza takwimu za ukuwaji wa uchumi wa taifa hilo kutoka asilimia 1.7 hadi 0.9.
Alikiri kwamba uchumi unazorota kutokana na kupungua kwa ukuaji wake, asilimia 25 ya ukosefu wa ajira na kuenea kwa umasikini.
Sarufi ya Afrika kusini Rand ambayo imeshuka katika kipindi cha miaka mitano ilianguka tena wakati alipokuwa akitoa hotuba hiyo.
Bwana Gordhan alitangaza kuongezeka kwa viwango vya kodi ya ushuru, faida ya mtaji, mafuta, vinywaji vyenye sukari, pombe na tumbaku pamoja na ushuru wa mazingira ambao unatarajiwa kuleta randi bilioni 18 sawa na dola bilioni 1.18.
Alikuwa ametarajiwa kutangaza mipango ya kubinafsisha mali ya serikali,lakini alisema kuwa mipango inaendelea ya kuunganisha shirika la ndege la taifa hilo lenye hasara na shirika la ndege linalomilikiwa na serikali la SA Express.
Morales ashindwa katika kura ya maoni.
Rais wa Bolivia Evo Morales ameshindwa katika juhudi zake za kutaka muhula wa nne madarakani, ikiwa ni kushindwa kwake kwa mara ya kwanza katika uchaguzi tangu kuingia madarakani mwaka 2006.
Morales mwenye umri wa miaka 56, amekuwa madarakani kwa muongo mmoja, akiungwa mkono zaidi na makundi ya wazalendo pamoja na matawi ya vijijini katika nchi hiyo masikini zaidi katika bara la Amerika.
Wakati akikataa kukubali matokeo hadi mwisho, Morales ameahidi kuheshimu matokeo rasmi baada ya uchaguzi wa hapo Jumapili kuhusiana na mabadiliko katika katiba ambayo yangemruhusu kugombea tena na kurefusha utawala wake hadi miaka 19. Kipindi chake cha sasa cha utawala kinamalizika mwaka 2020.
Wakati asilimia 99.72 za kura zimekwisha hesabiwa , rais wa tume ya uchaguzi Katia Uriona amesema kwamba asilimia 51.3 ya wapiga kura wamesema hapana katika kura hiyo ya maoni, dhidi ya asilimia 48.7 ambao wamesema ndio.
Subscribe to:
Posts (Atom)