Monday, November 30, 2015

JIPATIE HUDUMA ZA ARTS, GRAPHIC DESIGNS, NA TEXTILE DECORATION.

















najua mtakuwa mnajiuliza ni sehemu gani inaweza kukidhi mahitaji yako kama kuhitaji kugegsin vitu mbalimbali ikiwemo kuprint tshirt nk.


jibu lako ni PRO SIGNS BAGAMOYO hawa ni wataalamu waliobobea katika kazi hizi, ukihitaji kuwaona wapo mjini bagamoyo karibu na bagamoyo stand mabala na KINDAMBA RESTAURANTS.

Utafiti:Ulaji wa miraa unapunguza nguvu za kiume

 
 Ulaji wa Miraa unaathiri nguvu za kiume, Utafiti
Ulaji wa Miraa unaathiri nguvu za kiume.
Utafiti uliofanywa kwa niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa chuo kikuu cha Moi kilichoko katika Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya miraa inayofahamika pia kama 'Mairungi' unazuia ukuaji wa manii.
Aidha ulaji wa kipindi kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi zinapowekwa kwenye uke.
Mtafiti mkuu wa chuo kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa na huo uliofanywa huko ghuba ulibaini matokeo kama hayo.
Lukanda anasema kuwa wanaume ambao wamekuwa wakila Miraa kwa kipindi kirefu na wakaacha huwa wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.
Ulaji wa Miraa pia huwa unasababisha mshtuko wa moyo.
''Mtu anapokula mmea huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi, mbali na shinikizo la damu mumea huu hausababishi saratani kama inavyodaiwa '' Dakta Lukanda
 
 
Idadi ya vijana wanaokataa kwenda shule kwa sababu ya kujishughulisha na uchumaji upakiaji wa matawi yake.
Hata hivyo utafiti katika maeneo yanayokuzwa mumea huu umetambua kuwa idadi ya vijana wanaokataa kwenda shule kwa sababu ya kujishughulisha na uchumaji wa Miraa na upakiaji wa matawi yake.
''kutokana na utashi wa bidhaa hiyo,malipo ya wafanyikazi wanaoishughulikia ni ya juu mno kwa hivyo inawavutia vijana kuacha masomo alisema daktari huyo.
Daktari Lukoye Atwoli alisema kuwa miraa husababisha walaji wake kuwa na mori na hata wakati mwengine msongo wa mawazo.
Utafiti huu unafwatia ule uliofanywa mwaka uliopita na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Konstanz cha Germany na kile cha Minnesota, Marekani uliobaini kuwa ulaji wa miraa unaathiri ubongo wa walaji wake na kusababisha msongo wa mawazo,mafadhaiko na mahangaiko ya kiakili mbali na matatizo mengine chungu nzima.

gazeti la China lililomuandika Rais John Pombe Magufuli.


Wachimba mgodi 5 wafariki Geita Tanzania

 
Wachimbaji dhahabu watano wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi huko Geita
Wachimbaji dhahabu watano wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Mgusu mkoani Geita, Kusini Kaskazini mwa Tanzania.
Mwandishi wa BBC Sammy Awami anaarifu kuwa ,tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili katika machimbo yanayomilikiwa na kampuni ya Geita Gold Mine ambayo ni moja ya makampuni makubwa ya uchambaji wa dhahabu barani Afrika.
Makamu wa rais wa kampuni hiyo Simon Shayo ameiambia BBC kwamba miili hiyo iliokolewa jana kwa ushirikiano na wachimbaji wengine wa eneo hilo.
Shayo alisema eneo ambalo tukio hilo lilitokea si eneo salama na kwamba lilipigwa marufuku kwa shughuli za uchimbaji.
Hata hivyo baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiendelea kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji kinyemela na kupuuza ilani ya kutoingia katika maeneo hayo.
 
Wiki mbili tu zilizopita, wachimbaji wengine watano waliokolewa wakiwa hai katika machimbo ya Nyangalata baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku 41.
Wiki mbili tu zilizopita, wachimbaji wengine watano waliokolewa wakiwa hai katika machimbo ya Nyangalata baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku 41.
Wanne wao bado wako hospitalini, wakati mmoja alifariki dunia wiki iliyopita.

Kipigo cha Ethiopia chawarejesha Kilimanjaro Stars Tanzania, Full Time ya CECAFA Nov 30

Michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameendelea leo November 30 kwa kupigwa mechi za kwanza za robo fainali ya michuano hiyo, miongoni mwa mechi za robo fainali zilizochezwa leo November 30 ni mechi kati ya timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ilicheza dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ethiopia.
EthiopiaStars
Hii ni mechi ya robo fainali iliyokuwa inazikutanisha timu zilizokuwa kundi moja na mchezo wao wa mwisho walicheza na kumaliza kwa sare ya goli 1-1, November 30 Kilimanjaro Stars ilicheza mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili lakini kilikuwa na mabadiliko kidogo. Mchezo huo ambao Kilimanjaro Stars walianza kwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa nahodha wao John Bocco dakika ya 24, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya goli 1-1 baada ya Panom Cathuoch kuisawazishia goli Ethiopia dakika 57.
Ethiopia-cecafa
Kwa kawaida ya michuano hiyo kwa mechi za robo fainali umaliziwa kwa mikwaju ya penati kama dakika 90 zitamalizika kwa sare yaani bila kupata mshindi, hapo ndipo Kilimanjaro Stars ilikosa bahati na Ethiopia kufuzu hatua inayofuata kwa kwa kufanikiwa kushinda jumla ya penati 4-3.

Papa awataka Wakristo wasilipize kisasi

 

Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya Wakristo na Waislamu.
Papa Francis alikutana na Waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa kikristo waliojihami vikali wa Anti-Balaka.
Asili mia kubwa ya takriban waislamu laki moja nchini humo, walikimbia mji huo kufuatia mapigano yaliyodumu kwa ziaidi ya miaka mitati.
 
''Wakristo na Waislamu ni ndugu,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
Misikiti mingi iliharibiwa wakati wa vita hivyo.
Papa Francis amewataka wasameheane na waache kulipiza kisasi.
''Wakristo na Waislamu ni ndugu ,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
Image copyright Getty
Image caption Papa anaongoza misa yake ya mwisho katika uwanja wa taifa
''hatupaswi kulipiza kisasi na kumdhuru mtu yeyote kwa jina la mungu'' alisema Papa Francis.
Hivi sasa leo Papa Francis anaongoza misa yake ya mwisho barani Afrika katika uwanja mkuu wa kitaifa ambako anatarajiwa kutoa wito wa maridhiano, amani na utengamano.

Papa 'wakristu wasilipize kisasi' Afrika ya Kati

 
 
Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu.
Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa Anti-Balaka.
Asili mia kubwa ya takriban waislamu laki moja nchini humo, walikimbia mji huo kufuatia mapigano yaliyodumu kwa ziaidi ya miaka mitati.
 
 
''Wakristo na Waislamu ni ndugu,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
Misikiti mingi iliharibiwa wakati wa vita hivyo.
Papa Francis amewataka wasameheane na waache kulipiza kisasi.
''Wakristo na Waislamu ni ndugu ,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
Image copyright Getty
Image caption Papa anaongoza misa yake ya mwisho katika uwanja wa taifa
''hatupaswi kulipiza kisasi na kumdhuru mtu yeyote kwa jina la mungu'' alisema Papa Francis.
Hivi sasa leo Papa Francis anaongoza misa yake ya mwisho barani Afrika katika uwanja mkuu wa kitaifa ambako anatarajiwa kutoa wito wa maridhiano, amani na utengamano.

Maelezo kwenye kamera

Unaweza kutumia maelezo yako mwenyewe kwenye kamera kuonyesha ukubwa, umuhimu au wakati ambao umepita.

Watazamaji wanataka kujua kuwa upo katika eneo ambako jambo linatokea
Na wanataka kujua jinsi ilivyo kuwa hapo, kama anavyoeleza, mwandishi wa BBC wa maswala ya sayansi na mazingira David Shukman katika video hii:
Njia bora ya kutimiza hilo ni maelezo yako mwenyewe kwenye kamera.
Na si hilo tu. Unaweza kutumia maelezo yako mwenyewe kwenye kamera kuonyesha ukubwa, umuhimu au wakati ambao umepita.
David anashauri hivi:
  • Chagua jambo fulani muhimu katika taarifa yako ambalo unaweza kulieleza vyema zaidi kwenye kamera. Kwa mfano unaweza kujitumia wewe mwenyewe kuonyesha urefu, kimo au ukubwa wa kitu Fulani
  • Hakikisha unaangalia kamera wakati wote. Kuangalia kando huenda kukawasilisha maana tofauti, kwa hivyo fanya hivyo iwapo tu unataka kuwasilisha ujumbe Fulani
  • Vaa mikrofoni ya redio ili kuepuka kupaaza sauti sana, isipokuwa wakati unataka kelele za matukio kusikika
  • Tumia lugha ya kawaida na ya mazungumzo – kana kwamba unaongea na rafiki
  • Usiandike utakachosema kwenye kamera , badala yake fikiria njia ya kuanza, kumalizia na maneno yoyote muhimu
  • Tembea tu iwapo kuna kitu unataka kuonyesha, la sivyo usisonge. Songa tu wakati unataka kuonyesha uhusiano kati ya vitu au maeneo fulani.
  • Tumia vitu vinavyoweza kusaidia kueleza. Wakati mwingine unaweza kushika tunda au jiwe kurahisisha jambo gumu.

Israel yadai kubaguliwa na Palestina

 
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Israel imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na wawakiishi kutoka umoja wa ulaya wanaohusika na jitihada za kuleta amani kati ya Israel na Palestina.
Hatua hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu wiki mbili baada ya EU kuidhinisha sheria mpya kuhusu bidhaa zinazotoka Makazi ya waisraeli,Ukingo wa Magharibi.
Sheria hizo zinakataza bidhaa zilizo na nembo inayoonyesha kuwa zimetengenezwa Israel.
Hatua hii imesababisha ghadhabu kutoka kwenye seikali ya Israeli ambayo imesema sheria hizo ni za kibaguzi .

Magazeti ya Tanzania November 30 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho

Leo  November 30 2015 nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu, usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

EU, Uturuki zakubaliana suala wakimbizi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Umoja wa ulaya na uturuki wafikia makubaliano ya jinsi ya kuchukua hatua ili kuondokana na mafuriko ya wakimbizi na wahamiaji ndani ya bara la Ulaya, mkutano huo umefanyika nchini Ubeljiji katika makao maku ya EU.
Chini ya makubaliano hayodolla bilioni 3 zitatolewa na Umoja huo(EU) ili kusaidia wakimbizi kutoka nchi ya Syria wanaoelekea Uturuki.
Tayari Ankara imeshatumia dolla billioni 8 kutatua matatizo mbali mbali ya wageni hao.
Mazungumzo hayo yali fufua pia mjadala ju ya Uturuki kujiunga katika nchi zenye kuunda Umoja wa Ulaya na likazungumzwa pia la nchi hiyo kusafiri bila mipaka ndani ya bara hilo katika maeneo yaliyokubaliwa kutumia visa moja iitwayo shcenghen.
Waziri mku wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema ni tukio la kihistoria katika mahusiano ya ututruki na Umoja wa Ulaya.

Bomoabomoa yaendelea Dar, unawezaje kukwepa nyumba yako isibomolewe? majibu yako hapa.


Zoezi la kubomoa nyumba na majengo yaliyoingia ndani ya hifadhi ya miundombinu ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini, limeendelea mwishoni mwa wiki ambapo baaadhi ya nyumba zilizokuwa zimejengwa ndani ya maeneo hayo ya Salasala zimevunjwa.
01 copy
Katapila likiwa ndani ya gari tayari kwa kazi ya bomobomoa eneo la Salasala ,Dar es salaam 
Watu wengi wamekuwa hawaelewi vigezo vinavyozingatiwa hususani umbali sahihi wa mtu kujenga nyumba yake, hapa Mkurugenzi wa usimamizi na ufundi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang’ingo  anaeleza>>
Umbali sahihi unaopaswa wakazi hao kujenga makazi yao kutoka lilipo bomba la maji ni mita 15 kila upande ambapo hatua hiyo inapelekea kuwa jumla ya mita 30 ya umbali unaotakiwa
ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama na kuruhusu matengenezo mengine tofauti na hali ya awali ambayo huwezi hata kufanya kazi maana bomba limepita ndani ya uzio na makazi ya watu ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha yao na mali zao”;-Romanus Mwang’ingo
Maeneo yaliyohusishwa na ubomoaji huo ni pamoja na Bunju, Bondeni, Boko, Tegeta, Mbezi Intacheki, na Mbezi Tangibovu ili kuruhusu kukamilisha ujenzi wa bomba hilo la maji kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam.
02 copy
09 copy
Baadhi ya wakazi wa eneo la Salasala, Dar es salaam wakishuhudia zoezi la bomoabomoa
10 copy

Viongozi kujadili athari za joto duniani

 
 
 Wanaharakati wakiandamana Ujerumani kutaka hatua zichukuliwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
Mazungumzo kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.
Akifungua mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano chanya.
Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

Rais Magufuli na vigogo TRA, UDA na siku 30, Rais JPM avunja rekodi Baraza la Mawaziri, Meya DSM?


Good Morning mtu wangu? Kuperuzi na Kudadisi ya @CloudsFM imekupita? Kama umepitwa na dakika 20 za uchambuzi wa magazeti redioni leo asubuhi hizi ni baadhi ya stori zilizogusa headlines kwenye kurasa za leo.
Kasi ya Rais Magufuli yavunja ngome UKAWA, kasi ya kutumbua matibu yawafanya vigogo kubadili majina ya mali zao, waliojifanya miungu watu sehemu za kazi sasa wajishusha, Rais Dk John Magufuli avunja rekodi Baraza la Mawaziri wananchi walisubiria kwa hamu… wananchi wasubiri jibu la vinara wa  biashara ya dawa ya kulevya. Mali za vigogo wa TRA za ibua mjadala mkubwa huku mmoja akutwa na nyumba 73.
Shirika la Usafiri Dar es salaam, UDA ni moja ya mashirika yaliotajwa na kupewa siku 30 na Rais Magufuli kutoa maelezo ya kina kuhusu uwekezaji wake kabla ya kurejeshwa kwenye mikono ya Serikali, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mikataba ya uwekezeaji imekeukwa kwa kutoendelezwa mali hizo zilizokuwa za umma.
Vigogo wengi wa Serikali wanaotuhumiwa kujihisihsha na ubadhilifu wa fedha za umma na kuzitumia kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo nyumba za kisasa na kuzipangisha wameanza kubadilisha majina yao ili umiliki wao usifahamike.
Jiji la Dar es salaaam kuwa chini ya Meya anaetokea kwenye umoja wa UKAWA kwa mara ya kwanza… Bohari la dawa, MSD imejiimarisha na kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha kunakuwa na maduka ya dawa ndani ya hospitali zote za Serikali hapa nchini ambapo imeanza kwa kasi kubwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili.
Kampuni ya madini ya Petra Diamonds, imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pink yenye uzito wa karati 23.16 kutoka kwenye mgodi wake wa Wiliamson uliopo Shinyanga, almasi hiyo ni moja ya madini ya rangii yanayosakwa zaidi duniani na hupatikana kwenye migodi michache sana duniani.

Thursday, November 26, 2015

SLADS BAGAMOYO: WANACHUO WA CHUO CHA SLADS KUCHAGUA VIONGOZI WAO WAPYA LEO HII.

ni baada ya serikali ya HOSEA KAZIKUBOMA kumaliza mda wake madarakani na leo hii wanachuo hao wanaenda kuwachagua viongozi wapya.

LIST YA WAGOMBEA KATIKA NAFASI MBALIMBALI.



TING MEDIA ITAKUWA LIVE ILI KUKUSOGRZEA INTERVIEWS ZOTE ITAKAZOZIFANYA NA VIONGOZI HAO.

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa
Mwanaume mmoja aliyeua mkewe na kuchapisha picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook amepatikana na hatia ya mauaji.
Derek Medina mwenyeji wa Florida Marekani alipatikana na hatia ya kumpiga risasi 8 Jennifer Alfonso nyumbani kwao baada ya majibizano makali.
Kiongozi wa mashtaka wa jimbo la Miami-Dade,Katherine Rundle amesema inaudhi kuwa mwanamme mkatili anaweza kumpiga risasi mwanamke na kisha kuchapisha picha kwenye mtandao wa kijamii.
 
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
 
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
Aidha mwanaume huyo alivutia hisia kali baada ya kuchapisha picha ya mkewe akiwa anagaagaa sakafuni baada ya kumpiga risasi akisema anatarajia kufungwa kwa muda mrefu kwa kosa la kuua.
Kiongozi wa mashtaka ameiomba mahakama hiyo huko Miami kumhukumu mwanaume huyo Medina, 33, kwa miaka 25 jela kwa mauaji hayo.

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa
Mwanaume mmoja aliyeua mkewe na kuchapisha picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook amepatikana na hatia ya mauaji.
Derek Medina mwenyeji wa Florida Marekani alipatikana na hatia ya kumpiga risasi 8 Jennifer Alfonso nyumbani kwao baada ya majibizano makali.
Kiongozi wa mashtaka wa jimbo la Miami-Dade,Katherine Rundle amesema inaudhi kuwa mwanamme mkatili anaweza kumpiga risasi mwanamke na kisha kuchapisha picha kwenye mtandao wa kijamii.
 
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
Aidha mwanaume huyo alivutia hisia kali baada ya kuchapisha picha ya mkewe akiwa anagaagaa sakafuni baada ya kumpiga risasi akisema anatarajia kufungwa kwa muda mrefu kwa kosa la kuua.
Kiongozi wa mashtaka ameiomba mahakama hiyo huko Miami kumhukumu mwanaume huyo Medina, 33, kwa miaka 25 jela kwa mauaji hayo.

Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa

 
 
Mtoto mchanga apatikana katika hori la kanisa moja mjini New York Marekani
Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Yesu Kristu alizaliwa kwenye hori mjini Bethlehem.
Na katika tukio ambalo ni linafanana na hilo mtoto mdogo ambaye alikuwa kwenye hori amepatikana ndani ya kanisa moja mjini New York.
Inaaminika kuwa mtoto huyo mchanga ambaye ni mvulana aliachwa na mama yake, katika eneo takatifu la kanisa hilo siku ya Jumatatu jioni.
Mtoto huyo alipatikana na padre Christopher Heanue anayesimamia kanisa hilo.
Padre huyo amesema alishangazwa sana na tukio hilo ila alijawa na huruma nyingi.
Amesema kanisa ni mahala ambako watu wanaohitaji misaada na makao huenda na kwa kuwa papa Francis amekuwa akihubiri na kuhimiza waumini wote wawe na huruma, na zaidi ya yote mwaka huu ni mwaka wa huruma, amefarajika sana kuumpa mvulana huyo matumaini na mahala pa kuishi kwa kuwa anahitaji huruma na malezi.
Inaaminika kuwa mtoto huyo alikuwa amezaliwa chini ya saa tano wakati alipopatikana ndani ya kanisa hilo.
Mapadre wa kanisa hilo walimpeleka hospitalini kwa uchunguzi na inasemekana kuwa mtoto huyo yuko katika hali nzuri kiafya.
Askofu wa jimbo na New York Octavio Cisneros amesema mtoto huyo alikuwa amefunikwa na taulo na alikuwa akilia ishara tosha kuwa alikuwa salama wa siha .
 
 
Askofu wa jimbo na New York Octavio Cisneros amesema mtoto huyo alikuwa amefunikwa na taulo na alikuwa akilia ishara tosha kuwa alikuwa salama wa siha
Aidha alikuwa akipumua vyema na rangi yake ilikuwa sawa na kuwa waligundua kitovu chake hakikuwa kimekatwa.
Chini ya sheria za mji wa New York, kanisa ni mahala salama ambako mtu anaweza kumuacha mtoto wake ambaye ana zaidi ya siku thelathini.
hata hivyo mama wa mtoto huyo ni sharti amjulishe mtu yeyote kuwa amemuacha mtoto ndani ya kanisa ili awajulishe wasimamizi wa kanisa hilo au maafisa wa utawala.
Mama mzazi wa mtoto huyo tayari amepatikana na amehojiwa na polisi.
Mwendesha mashtaka wa mji huo amesema mama huyo hatafunguliwa mashtaka yoyote ya kihalifu kwa sababu alimucha mtoto wake katika hali nzuri na eneo linalokubalika kisheria.

Hizi ndio rekodi 4 za nguvu alizoweka Rais Magufuli siku ya alhamis


Leo ni siku ya alhamisi, November 26 2015… nimeinasa hii ripoti exclusive kabisa iliyoripotiwa na kituo cha Clouds TV, kama ulikuwa hujui basi kuna rekodi kubwa na za nguvu kabisa ambazo zinaihusu siku ya alhamisi na Rais John Pombe Magufuli.
Hapa nakuchambulia mdogomdogo mtu wangu, mwanzo mpaka mwisho wa rekodi zenyewe.
1:>> Rais Magufuli alizaliwa October 29 1959, ilikuwa ni siku ya alhamisi.
2:>> October 29 2015 ni siku ambayo alitangazwa kuwa Rais wa Tanzania… ilikuwa alhamisi pia.
3:>> Siku ya alhamisi November 05 2015 Rais Magufuli aliapishwa kushika wadhifa wa Urais wa Tanzania, Ikulu Dar es Salaam.
4:>> November 19 2015, Rais Magufuli alimteua Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Urusi kushirikiana kupambana na IS

 
 Rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenziye wa Ufaransa Francois Hollande
Urusi imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.
Rais Vladmir Putin amemwambia mweziye wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo.
Rais huyo wa Ufaransa yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini Syria.

Adam Juma kayaandika haya kwa madirector wenzake……


Muongozaji wa video za Bongo Adam Juma leo ameandika ujumbe ambao inawezekana ukawahusu baadhi ya waongozaji wengine wa video za Tanzania.
Kwa madirector wadogo na wakubwa, hakuna mafanikio yanakuja kirahisi rahisi, hakuna media itakayokuokoa katika ukame wa kazi utakapo wasili. Sifa hujenga kiburi akili hujenga ustaarabu, mafanikio yako yapo mkononi mwako- hata wakishoot mbinguni isiwe sababu ya wewe kuacha na kutoipenda kazi yako‘ – Adam Juma
Simama kwenye mstari na ujiamini, usishindane na upepo wa dunia hautashinda. Hakuna anayeweza akawa namba 1 kila siku na ukilijua hili utalala vizuri bila mawazo. Kila kazi ya mikono yangu ni zawadi kwa atakayeipenda na kuichukia, najiamini na naipenda kazi yangu. Ubunifu ndio utakao tuokoa katika ukame huu na sio budget, uongo, chuki na majigambo. Stay blessed all’Adam Juma

Papa Francis aonya kuhusu ongezeko la joto

 
 Ziara ya Papa Francis Kenya
Papa Francis amesema ni jambo la aibu kama viongozi wa dunia hawatafikia muafaka juu ya namna ya kupambana na ongezeko la joto duniani.
Akizungumza katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP) mjini Nairobi, Alhamisi kiongozi huyo wa Kanisa katoliki duniani alisema maslahi ya watu fulani hayapaswi kuruhusiwa kutawala badala ya manufaa ya wote.
Kabla ya kuzungumzia hayo Papa Francis alikutana na viongozi wa dini ili kujadili umuhimu wa mazungumzo, na kuwa na misa za wazi kabla kukutana na umati wa maelfu ya waumini katika mji mkuu wa Kenya.
Katika ziara yake barani Afrika, kiongozi mkuu huyo wa Kanisa Katoliki amepangiwa kuelekea nchini Uganda leo na kuimalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati Novemba 30.

Magazeti ya Tanzania November 27 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho


Leo  November 27 2015 nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu, usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Wednesday, November 25, 2015

SLADS BAGAMOYO: BAADA YA DIPLOMA TWO GREEN KUIBUKA KIDEDEA KATIKA FAINA...

SLADS BAGAMOYO: BAADA YA DIPLOMA TWO GREEN KUFUNGA GOLI LA PILI.

SLADS BAGAMOYO; KIDEDEA CHA DIPLOMA TWO GREEN PART TWO

SLADS BAGAMOYO: KIDEDEA CHA DIPLOMA TWO GREEN.

SLADS BAGAMOYO: DIPLOMA TWO GRENN WAKIWA WANAJIANDAA NA MPAMBANO NA DAR ...

SLADS BAGAMOYO: MOJA KATI YA NAFASI ZA MAGOLI WALIZOZIPATA NA KUZIKOSA D...

Kilichoamuliwa na mahakama kuu Mwanza kuhusu kesi ya marehemu Alphonce Mawaz.

 

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo iliendelea kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Charles Rugiko ambaye ni ndugu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kwa  kupinga zuio la jeshi la polisi kuchukua na kuaga mwili wa ndugu yao kwa maelezo ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini..
Zuio  hilo lilitolewa na RPC mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo tangu November 14 mwaka 2015.
Hatimaye mahakama hiyo  imefikia uamuzi wa kuisogeza kesi hiyo hadi hapo kesho Novemba 26 ambapo inatarajiwa hukumu kutolewa rasmi.
Millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na wakili  wa Chadema John Mallya pamoja na naibu katibu wa Chadema Salum Mwalimu.
Na hapa naibu katibu mkuu anazungumza>>
Pande zote mbili zimemaliza kuwasilisha hoja zao, imeamuliwa kesho tukutane saa saba, mwenendo unarithisha na ni imani yetu kuwa haki itapatikana”;- Salum Mwalimu
Hatutarajii baada ya hukumu kutaendelea kutokea tena kwa vitendo kama hivi, lai yetu kama chama na familia ni kwamba tuendelee kutunza amani na utulivu kwakuwa ndio jadi yetu” ;- Salum Mwalimu
Tunawaomba ndugu na mashabiki wetu waendelee kutunza amani hadi hapo kesho saa 7 tutakapo kuja kupata hatma na tutaelezana utaratibu mpya, na tuendelee kuionyesha dunia kuwa Chadema ni watu wa amani ” ;- Salum Mwalimu
DSC_0095
Kwa upande wake mwanasheria wa Chadema John Mallya akayasema haya>> “pande zote mbili zimetoa hoja ya msingi ya kwanini  sisi tunaomba maombi yetu na upande wa jamuhuri wametoa yao ya kwanini wao wanaona tusipewe maombi yetu, mabishano yalikuwa makali, mheshimiwa jaji ameenda kuandika hukumu na kesho saa saba tutapata uamuzi wa jaji juu ya jambo hili huku tukiamini haki itatendekaJOHN MALLYA
DSC_0102

Gambia yapiga marufuku tohara ya wanawake

Gambia yapiga marufuku tohara ya wanawake
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh,amepiga marufuku tohara ya wanawake nchini humo akisema inakwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.
Umoja wa mataifa unasema karibu robo tatu za wanawake wa Gambia wamefanyiwa ukeketaji.
Watabibu wamekuwa wakieleza matatizo ya kiafya yanayotokea kutokana na tabia hiyo lakini hilo halijapunguza visa vya upashaji tohara wanawake nchini hiumo.
 
Madaktari wamekuwa wakielezea matatizo ya kiafya yanayotokana na kupashwa tohara kwa wanawake
Sasa rais Yahya Jameh amesema amekuwa akitafiti kwa muda wa miaka 21 katika kitabu tukufu cha Quran na vilevile kupitia mahojiano na wanazuoni wa kiislamu na hamna ushahidi wowote wa kufungamanisha kitendo hicho na dini ya Kiislamu.