Thursday, November 26, 2015

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa

Aliyeua na kuchapisha kwa Facebook kufungwa
Mwanaume mmoja aliyeua mkewe na kuchapisha picha yake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook amepatikana na hatia ya mauaji.
Derek Medina mwenyeji wa Florida Marekani alipatikana na hatia ya kumpiga risasi 8 Jennifer Alfonso nyumbani kwao baada ya majibizano makali.
Kiongozi wa mashtaka wa jimbo la Miami-Dade,Katherine Rundle amesema inaudhi kuwa mwanamme mkatili anaweza kumpiga risasi mwanamke na kisha kuchapisha picha kwenye mtandao wa kijamii.
 
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
 
Medina alidai kuwa mkewe mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ametishia kumdunga kisu.
Aidha mwanaume huyo alivutia hisia kali baada ya kuchapisha picha ya mkewe akiwa anagaagaa sakafuni baada ya kumpiga risasi akisema anatarajia kufungwa kwa muda mrefu kwa kosa la kuua.
Kiongozi wa mashtaka ameiomba mahakama hiyo huko Miami kumhukumu mwanaume huyo Medina, 33, kwa miaka 25 jela kwa mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment