Sunday, November 22, 2015
SLADS BAGAMOYO: ATOA MACHOZI BAADA YA TIMU YAKE KUONDOLEWA KATIKA MCHUANO. ni mcezaji wa timu ya diploma 2 pink (masudy) jana ametoa chozi lake nje baada ya timu yake kutupwa nje ya michuano ya SLADS INTERCLASS na diploma 2 green. DIPLOMA TWO GREEN. jana ilikuwa ni nusu fainali ya pili mchezo uliowakutanisha watani wa jadi kwa mara nyingine tena DIPLOMA 2 PINK NA GREEN.mchezo huo ulikuwa ni mchezo wa kukamiana ambapo kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu hizo kufungana, timu zilirudi kipindi cha pili kwa mabadiliko makubwa na ndipo mchezaji moja wa timu ya green alipofanyiwa madhambi nje ya lango la diploma 2 pink na mwamuzi akaamuru faulu ipigwe kuelekezwa katika lango la timu ya pink, na faulu hiyo ndiyo iliweza kuleta matunda ya goli moja, faulu hiyo iliwekwa kimiani na mchezaji machachali fredy kivike, mpaka mpira unamalizika diploma two green bao moja na diploma 2 pink sifuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment