Monday, November 16, 2015

Kama ulipitwa, kuna hii nyingine.. watu waliofukiwa na kifusi siku 41 na wametoka hai Kahama..!!


Moja ya stori kubwa niliyokutana nayo leo ni hii ambayo imeripotiwa kwenye habari Kituo cha ITV ambayo inahusu taarifa kutoka wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga… kilichoipa uzito zaidi hii taarifa ni ishu ya watu watano kati ya sita waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo ya Nyangarata kwa siku 41, wameokolewa wakiwa hai.
IMAG0755
Watu hao walifukiwa wakiwa kwenye harakati za kuokoa wenzao waliokuwa wamenasa kwa kufukiwa na kifusi, hii ni sehemu ya kilichosemwa na mmoja wa watu ambao walifukiwa na wametoka hai >>> “tulikuwa tumebaki watu sita chini, tukawa tunakunywa maji tuliyoyakanyaga na kuyakojolea, tulikula magome ya miti, mende pamoja na vyura” >>> Joseph Burure.
IMAG0749
Wenyeji wa eneo hilo wamesema walikuwa kwenye jitihada za kuitoa miili ya watu hao kutoka ndani ya machimbo ambapo walihisi kwamba wamefariki, ila baadae wakagundua kwamba kuna watu walionasa chini, ikabidi waanze taratibu za kuwatoa, wakawakuta wakiwa hai huku wakiwa na upungufu mkubwa wa maji mwilini pamoja na majeraha… mmoja kati ya watu hao alifariki, watano wakatoka hai.

No comments:

Post a Comment