Adam Juma kayaandika haya kwa madirector wenzake……
Muongozaji
wa video za Bongo Adam Juma leo ameandika ujumbe ambao inawezekana
ukawahusu baadhi ya waongozaji wengine wa video za Tanzania.
‘Kwa
madirector wadogo na wakubwa, hakuna mafanikio yanakuja kirahisi
rahisi, hakuna media itakayokuokoa katika ukame wa kazi utakapo wasili.
Sifa hujenga kiburi akili hujenga ustaarabu, mafanikio yako yapo mkononi
mwako- hata wakishoot mbinguni isiwe sababu ya wewe kuacha na
kutoipenda kazi yako‘ – Adam Juma
‘Simama
kwenye mstari na ujiamini, usishindane na upepo wa dunia hautashinda.
Hakuna anayeweza akawa namba 1 kila siku na ukilijua hili utalala vizuri
bila mawazo. Kila kazi ya mikono yangu ni zawadi kwa atakayeipenda na
kuichukia, najiamini na naipenda kazi yangu. Ubunifu ndio utakao tuokoa
katika ukame huu na sio budget, uongo, chuki na majigambo. Stay blessed
all’ – Adam Juma
No comments:
Post a Comment