Mvulana aliyetuhumiwa kuwa 'gaidi' adai fidia
Mvulana wa umri wa
miaka 14 aliyezoa umaarufu baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya
kujitengenezea shuleni, anadai fidia ya dola milioni 15 ($15m).
Ahmed
Mohammed alitiwa mbaroni na polisi wa mji wa Irving, jimbo la Texas
nchini Marekani baada ya saa yake kudhaniwa kuwa kilipuzi na baadaye
akafukuzwa shule.
Taarifa ya wakili wake inasema tukio hilo
lililogonga vichwa vya habari duniani, lilimfanya apokee vitisho na
kumsababishia matatizo ya kisaikolojia.
Ahmed na familia yake baadaye walihamia nchini Qatar ambapo anaendelea na elimu yake.
Kukamatwa
kwake kuliibua hasira na huruma, huku watumizi wa mtandao wa kijamii wa
Twitter wakitumia #StandWithAhmed kutoa tetesi zao.
Mawakili wake
wanadai dola milioni 10 kutoka kwa mji wa Irving na dola milioni 5
kutoka kwa shule ya Irving Independent School District, wakisema Ahmed
alifedheheshwa peupe na akaathirika kisaikolojia.
Kando na fidia,
mawakili wake wanadai kuombwa msamaha, wakisema baada ya tukio hilo,
Ahmed amekuwa akipokea jumbe za vitisho na kuwa anahofia usalama wake,
swala linalomletea matatizo ya kisaikolojia.
Mawakili hao wanasema watapeleka kesi ya kiraia mahakamani iwapo shule hiyo haitotimiza matakwa ya Ahmed kwa muda wa siku 60.
"maafisa
wa polisi wa Irving waligundua kwa haraka kuwa saa hiyo haingedhuru
yeyote. Saabu pekee ya kufanya walichofanya ni kwa sababu watu wazima
waliohusika bila umakini, walidhani Ahmed alikuwa mvulana hatari
kutokana na asili yake, taifa lake na dini". Mawakali wanasema kwenye
barua walioandikia mji wa Irving.
Ahmed aliambia wanahabari kuwa kwa wakati huo "ilisikitisha" kuwa mwalimu wake alidhani kuwa saa yake ilikuwa tisho.
No comments:
Post a Comment