Wachimba mgodi 5 wafariki Geita Tanzania
Wachimbaji dhahabu
watano wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya Mgusu
mkoani Geita, Kusini Kaskazini mwa Tanzania.
Mwandishi wa BBC
Sammy Awami anaarifu kuwa ,tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia
Jumapili katika machimbo yanayomilikiwa na kampuni ya Geita Gold Mine
ambayo ni moja ya makampuni makubwa ya uchambaji wa dhahabu barani
Afrika.Makamu wa rais wa kampuni hiyo Simon Shayo ameiambia BBC kwamba miili hiyo iliokolewa jana kwa ushirikiano na wachimbaji wengine wa eneo hilo.
Shayo alisema eneo ambalo tukio hilo lilitokea si eneo salama na kwamba lilipigwa marufuku kwa shughuli za uchimbaji.
Hata hivyo baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiendelea kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji kinyemela na kupuuza ilani ya kutoingia katika maeneo hayo.
Wiki mbili tu zilizopita, wachimbaji wengine watano waliokolewa wakiwa hai katika machimbo ya Nyangalata baada ya kufukiwa na kifusi kwa siku 41.
Wanne wao bado wako hospitalini, wakati mmoja alifariki dunia wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment