Monday, November 30, 2015

Rais Magufuli na vigogo TRA, UDA na siku 30, Rais JPM avunja rekodi Baraza la Mawaziri, Meya DSM?


Good Morning mtu wangu? Kuperuzi na Kudadisi ya @CloudsFM imekupita? Kama umepitwa na dakika 20 za uchambuzi wa magazeti redioni leo asubuhi hizi ni baadhi ya stori zilizogusa headlines kwenye kurasa za leo.
Kasi ya Rais Magufuli yavunja ngome UKAWA, kasi ya kutumbua matibu yawafanya vigogo kubadili majina ya mali zao, waliojifanya miungu watu sehemu za kazi sasa wajishusha, Rais Dk John Magufuli avunja rekodi Baraza la Mawaziri wananchi walisubiria kwa hamu… wananchi wasubiri jibu la vinara wa  biashara ya dawa ya kulevya. Mali za vigogo wa TRA za ibua mjadala mkubwa huku mmoja akutwa na nyumba 73.
Shirika la Usafiri Dar es salaam, UDA ni moja ya mashirika yaliotajwa na kupewa siku 30 na Rais Magufuli kutoa maelezo ya kina kuhusu uwekezaji wake kabla ya kurejeshwa kwenye mikono ya Serikali, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mikataba ya uwekezeaji imekeukwa kwa kutoendelezwa mali hizo zilizokuwa za umma.
Vigogo wengi wa Serikali wanaotuhumiwa kujihisihsha na ubadhilifu wa fedha za umma na kuzitumia kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo nyumba za kisasa na kuzipangisha wameanza kubadilisha majina yao ili umiliki wao usifahamike.
Jiji la Dar es salaaam kuwa chini ya Meya anaetokea kwenye umoja wa UKAWA kwa mara ya kwanza… Bohari la dawa, MSD imejiimarisha na kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati agizo la Rais Magufuli la kuhakikisha kunakuwa na maduka ya dawa ndani ya hospitali zote za Serikali hapa nchini ambapo imeanza kwa kasi kubwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili.
Kampuni ya madini ya Petra Diamonds, imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pink yenye uzito wa karati 23.16 kutoka kwenye mgodi wake wa Wiliamson uliopo Shinyanga, almasi hiyo ni moja ya madini ya rangii yanayosakwa zaidi duniani na hupatikana kwenye migodi michache sana duniani.

No comments:

Post a Comment