Somalia:7 wauawa wakisubiri chakula cha msaada
Polisi katika mji
mkuu wa Somalia Mogadishu wameripotiwa kuua watu saba wakati wa shuguli
ya mgao wa chakula cha msaada katika kambi moja ya wakimbizi.
Shahidi mmoja amesema wanawake ni kati ya waliouawa.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko amesema maafisa wa polisi walianza kugombana kabla ya kuanza kufyatuliana risasi.
Watu
wengine 12 walijeruhiwa katika makabiliano hayo baina ya maafisa
hasimu walipokuwa wakisubiri kugawanyia kadi na vibali vya kuwaruhusu
kupokea vyakula vya msaada.
''kulitokea ufyatulianaji wa risasi
kati ya maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda bohari la vyakula vya
msaada na maafisa wa jeshi''alisema Mohamed Burhan ambaye ni afisa wa
Polisi.
''raia 7 waliuawa katika makabiliano hayo nje ya Mogadishu''
Waliouawa ni pamoja na watoto na wanawake na wanaume wazee.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nick Kay
alielezea kughadhabishwa na mno na mauaji hayo ya watu waliokuwa na
njaa wakitafuta chakula cha msaada''
''Sharti haki ifanyike dhidi ya wale waliotekeleza mauaji hayo''
Mauaji hayo yalitokea mjini Afgoye nje ya mji mkuu wa Mogadishu.
Hadi kufikia sasa haijulikani ni nini kilichotibua makabiliano hayo.
Eneo hilo linadhibitiwa na serikali baada ya majeshi ya umoja wa Afrika kuwafurusha wapiganaji wa al Shabaab.
Maelfu ya wasomali waliotoroka makwao wangali wanaishi katika kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani nje ya Mogadishu.
No comments:
Post a Comment