Mali: Miili ya watu 18 imedaiwa kupatikana hotelini Polisi wa Mali wameingia katika hoteli
Maafisa wa serikali
ya Mali wamesema sasa hakuna mateka wowote waliosalia katika hoteli ya
Radisson Blu mjini Bamako iliyokuwa imeshambulia asubuhi na watu wenye
silaha huku miili ya watu 18 ikidaiwa kupatikana ndani ya hoteli hiyo.
Waziri wa usalama wa Mali Salif Traore ameambia kikao cha
wanahabari kwamba watu wenye silaha walioshambulia hoteli ya Radisson
kwa sasa hawazuilii mateka wowote.
Afisi ya rais wa Mali imeandika
kwenye Twitter ikishukuru maafisa wa usalama na mataifa yaliyosaidia
kukabiliana na shambulio hoteli hiyo ya kifahari.
Watu watatu wamethibitishwa kufariki na wanajeshi wawili kujeruhiwa.
Ubelgiji imesema afisa mmoja wa serikali yake ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo.
Geoffrey Dieudonne alikuwa Mali kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa serikali.
Uvamizi
huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa mapema asubuhi kwenye hoteli hiyo ya
kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.Radisson Blu Hotel
Image caption
Tovuti ya hoteli hiyo inaieleza kama "hoteli ya kifahari
Baadhi ya ripoti zilisema watu walioshambulia hoteli hiyo huenda wakafika 10.
Ufaransa ambayo
imekuwa na wanajeshi Mali tangu 2013 ilituma wanajeshi wake kusaidiana
na wanajeshi wa Mali. Aidha, polisi maalum wapatao 50 walitumwa kutoka
Paris.
Kundi la wapiganaji wa kijihadi la al-Murabitoun limedai
kuhusika kwenye shambulio hilo kupitia ujumbe kwenye akaunti ya Twitter
ya kundi hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ingawa habari
hizo hazijathibitishwa. Kundi la Al-Murabitoun linajumuisha makundi
mawili ambayo yalijitenga kutoka kwa tawi moja la al-Qaeda eneo la
Afrika Kaskazini.
Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13,
wakiwemo wafanyakazi watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu
katika mji wa Sevare, katikati mwa Mali.
Ubalozi wa Marekani mjini
Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo
na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na
familia.
No comments:
Post a Comment