Viongozi kujadili athari za joto duniani
Mazungumzo kuhusu
Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris
nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa
kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano
yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na
ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi
ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja
wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano
iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.
Akifungua mkutano
huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana
uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano
chanya.
Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha
Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la
kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois
Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini
waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.
No comments:
Post a Comment