Maelezo kwenye kamera
Unaweza kutumia maelezo yako mwenyewe kwenye kamera kuonyesha ukubwa, umuhimu au wakati ambao umepita.
Watazamaji wanataka kujua kuwa upo katika eneo ambako jambo linatokea
Na wanataka kujua jinsi ilivyo kuwa hapo, kama anavyoeleza, mwandishi wa BBC wa maswala ya sayansi na mazingira David Shukman katika video hii:
Njia bora ya kutimiza hilo ni maelezo yako mwenyewe kwenye kamera.
Na si hilo tu. Unaweza kutumia maelezo yako mwenyewe kwenye kamera kuonyesha ukubwa, umuhimu au wakati ambao umepita.
David anashauri hivi:
- Chagua jambo fulani muhimu katika taarifa yako ambalo unaweza kulieleza vyema zaidi kwenye kamera. Kwa mfano unaweza kujitumia wewe mwenyewe kuonyesha urefu, kimo au ukubwa wa kitu Fulani
- Hakikisha unaangalia kamera wakati wote. Kuangalia kando huenda kukawasilisha maana tofauti, kwa hivyo fanya hivyo iwapo tu unataka kuwasilisha ujumbe Fulani
- Vaa mikrofoni ya redio ili kuepuka kupaaza sauti sana, isipokuwa wakati unataka kelele za matukio kusikika
- Tumia lugha ya kawaida na ya mazungumzo – kana kwamba unaongea na rafiki
- Usiandike utakachosema kwenye kamera , badala yake fikiria njia ya kuanza, kumalizia na maneno yoyote muhimu
- Tembea tu iwapo kuna kitu unataka kuonyesha, la sivyo usisonge. Songa tu wakati unataka kuonyesha uhusiano kati ya vitu au maeneo fulani.
- Tumia vitu vinavyoweza kusaidia kueleza. Wakati mwingine unaweza kushika tunda au jiwe kurahisisha jambo gumu.
No comments:
Post a Comment