Utafiti:Ulaji wa miraa unapunguza nguvu za kiume
Ulaji wa Miraa unaathiri nguvu za kiume.
Utafiti
uliofanywa kwa niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa chuo kikuu
cha Moi kilichoko katika Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya miraa
inayofahamika pia kama 'Mairungi' unazuia ukuaji wa manii.Aidha ulaji wa kipindi kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi zinapowekwa kwenye uke.
Mtafiti mkuu wa chuo kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa na huo uliofanywa huko ghuba ulibaini matokeo kama hayo.
Lukanda anasema kuwa wanaume ambao wamekuwa wakila Miraa kwa kipindi kirefu na wakaacha huwa wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.
Ulaji wa Miraa pia huwa unasababisha mshtuko wa moyo.
''Mtu anapokula mmea huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi, mbali na shinikizo la damu mumea huu hausababishi saratani kama inavyodaiwa '' Dakta Lukanda
Hata hivyo utafiti katika maeneo yanayokuzwa mumea huu umetambua kuwa idadi ya vijana wanaokataa kwenda shule kwa sababu ya kujishughulisha na uchumaji wa Miraa na upakiaji wa matawi yake.
''kutokana na utashi wa bidhaa hiyo,malipo ya wafanyikazi wanaoishughulikia ni ya juu mno kwa hivyo inawavutia vijana kuacha masomo alisema daktari huyo.
Daktari Lukoye Atwoli alisema kuwa miraa husababisha walaji wake kuwa na mori na hata wakati mwengine msongo wa mawazo.
Utafiti huu unafwatia ule uliofanywa mwaka uliopita na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Konstanz cha Germany na kile cha Minnesota, Marekani uliobaini kuwa ulaji wa miraa unaathiri ubongo wa walaji wake na kusababisha msongo wa mawazo,mafadhaiko na mahangaiko ya kiakili mbali na matatizo mengine chungu nzima.
No comments:
Post a Comment