Friday, November 13, 2015

Michezo

Ijue siri ya rozari ya Joseph Kimwaga wa Simba, kwa nini anavaa muda wote? akiingia uwanjani je?


Jina Joseph Kimwaga sio geni katika soka la Tanzania hususani katika vilabu vya Azam FC na Simba, Kimwaga alianza kusikika katika soka akiwa katika klabu ya Azam FC kabla ya dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 kuomba kwenda katika klabu ya Simba kwa mkopo wa muda mrefu.
Kimwaga ambaye ana umri wa miaka 19 ni miongoni mwa mastaa chipukizi wa mchezo wa soka wanaofanya vizuri kwa sasa, stori za ushirikina katika soka zipo na zimewahi kumfikia Joseph Kimwaga ila yeye huwa anaamini katika dini yake ya kikristo na kuvaa rozari, licha ya kuwa rozari hukatazwa mchezaji kuvaa wakati wa mechi Kimwaga huwa anaifunga katika bukta yake ili refa asijue kwa imani yake anaamini inamlinda.
IMG_20151113_215912
Staa huyo ambaye amewahi kuingia katika headlines baada ya kufunga goli la ushindi kwa klabu yake ya Azam FC dhidi ya Yanga amepewa rozari hiyo iliyotoka kwa Papa kutoka Italia na padri wake, ndio aliompatia hivyo kwa sababu imebarikiwa na Papa sio rahisi kwa vitu vya imani za giza kumpata Kimwaga.
“Kuna majaribu ambayo yanatokea katika soka kiukweli ila kama una roho fupi unaweza ukaacha lakini ni vitu ambavyo mimi na imani kwa sababu nikikumbuka tu msemo mmoja nilioambiwa na paroko kuwa ukiingia tu katika imani ndio majaribu yatakavyozidi kwa hiyo mimi na imani na ndio maana navaa rozari muda wote” >>> Joseph Kimwaga

No comments:

Post a Comment