Wednesday, November 25, 2015

Kilichoamuliwa na mahakama kuu Mwanza kuhusu kesi ya marehemu Alphonce Mawaz.

 

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo iliendelea kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Charles Rugiko ambaye ni ndugu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kwa  kupinga zuio la jeshi la polisi kuchukua na kuaga mwili wa ndugu yao kwa maelezo ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini..
Zuio  hilo lilitolewa na RPC mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo tangu November 14 mwaka 2015.
Hatimaye mahakama hiyo  imefikia uamuzi wa kuisogeza kesi hiyo hadi hapo kesho Novemba 26 ambapo inatarajiwa hukumu kutolewa rasmi.
Millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na wakili  wa Chadema John Mallya pamoja na naibu katibu wa Chadema Salum Mwalimu.
Na hapa naibu katibu mkuu anazungumza>>
Pande zote mbili zimemaliza kuwasilisha hoja zao, imeamuliwa kesho tukutane saa saba, mwenendo unarithisha na ni imani yetu kuwa haki itapatikana”;- Salum Mwalimu
Hatutarajii baada ya hukumu kutaendelea kutokea tena kwa vitendo kama hivi, lai yetu kama chama na familia ni kwamba tuendelee kutunza amani na utulivu kwakuwa ndio jadi yetu” ;- Salum Mwalimu
Tunawaomba ndugu na mashabiki wetu waendelee kutunza amani hadi hapo kesho saa 7 tutakapo kuja kupata hatma na tutaelezana utaratibu mpya, na tuendelee kuionyesha dunia kuwa Chadema ni watu wa amani ” ;- Salum Mwalimu
DSC_0095
Kwa upande wake mwanasheria wa Chadema John Mallya akayasema haya>> “pande zote mbili zimetoa hoja ya msingi ya kwanini  sisi tunaomba maombi yetu na upande wa jamuhuri wametoa yao ya kwanini wao wanaona tusipewe maombi yetu, mabishano yalikuwa makali, mheshimiwa jaji ameenda kuandika hukumu na kesho saa saba tutapata uamuzi wa jaji juu ya jambo hili huku tukiamini haki itatendekaJOHN MALLYA
DSC_0102

No comments:

Post a Comment