Monday, November 30, 2015

Israel yadai kubaguliwa na Palestina

 
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Israel imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na wawakiishi kutoka umoja wa ulaya wanaohusika na jitihada za kuleta amani kati ya Israel na Palestina.
Hatua hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu wiki mbili baada ya EU kuidhinisha sheria mpya kuhusu bidhaa zinazotoka Makazi ya waisraeli,Ukingo wa Magharibi.
Sheria hizo zinakataza bidhaa zilizo na nembo inayoonyesha kuwa zimetengenezwa Israel.
Hatua hii imesababisha ghadhabu kutoka kwenye seikali ya Israeli ambayo imesema sheria hizo ni za kibaguzi .

No comments:

Post a Comment