Marekani yamshambulia Jihadi John
Wanajeshi wa
Marekani wametekeleza shambulio la kutoka angani lililomlenga
mwanamgambo wa Islamic State kutoka Uingereza ajulikanaye kama "Jihadi
John", Pentagon amesema.
Mohammed Emwazi,
Mwingereza aliyezaliwa Kuwait, alilengwa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria.
Msamo
mkali wa kumtafuta Emwazi ulianza baada ya mwanamgambo huyo kuonekana
katika video akiwakata shingo mateka wa kutoka mataifa ya Magharibi.
Pentagon bado inachunguza kubaini iwapo Emwazi ameuawa kwenye shambulio hiyo.
Afisa
wa habari wa Pentagon Peter Cook amesema: "Tunatathmini matokeo ya
operesheni ya leo usiku na tutatoa taarifa zaidi baadaye.”
Emwazi anaaminika kusafiri Syria 2013 na kisha akajiunga na wapiganaji wa Islamic State.
Alionekana
mara ya kwanza kwenye video Agosti mwaka jana, kanda ya video
ilipopakiwa mtandaoni ikionyesha mauaji ya mwanahabari wa Marekani James
Foley.
Baadaye alionekana kwenye video za kuuawa kwa mwanahabari
wa Marekani Steven Sotloff, mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada wa
Uingereza David Haines na dereva wa teksi kutoka Uingereza Alan Henning.
Aidha,
alikuwepo kwenye video ya kuuawa kwa mfanyakazi wa kutoa misaada kutoka
Marekani Abdul-Rahman Kassig, aliyejulikana pia kama Peter na
mwanahabari wa Japan Kenji Goto.
Katika kila video, alionekana akiwa amevalia kanzu nyeusi na barakoa nyeusi ya kufunika uso wake.
Awali
alijulikana tu kama "Jihadi John", lakini baadaye ikabainika kwamba
alikuwa ni Emwazi, kutoka magharibi mwa London, Februari
No comments:
Post a Comment