Wednesday, November 18, 2015

MCHUNGAJI KUWALISHA NYOKA WAUMINI NA NGUO ZA NDANI 

Hizi stori kutoka kwa viongozi wa nyumba za ibada kuwa na matendo yanayoibua maswali mengi sio ngeni masikioni mwetu, nimeinasa nyingine toka South Africa, Mchungaji kawalisha Waumini wake nyoka pamoja na nguo za ndani..
Penuel-Mnguni-of-End-Times-Disciples-Ministries-1
Mchungaji huyo Penuel Mnguni ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la End Times Disciples Ministries lililopo katika Mji wa Soshanguve ulioko Pretoria South Africa, alijikuta akiishia mikononi mwa watu wenye hasira na matendo yake, huku Kanisa lake likiteketea baada ya kuchomwa moto na watu haohao !!
Penuel-Mnguni-of-End-Times-Disciples-Ministries-2
Taarifa zilienea mitaani kuhusu huduma zake, alikuwa akiwalazimisha waumini wake kula nyoka pamoja na nguo za ndani kama sehemu ya huduma za Kanisa lake kwa Waumini… watu wa eneo hilo waliwavamia na kumkamata Mchungaji huyo, Kanisa likaishia kuchomwa moto, ambapo baada ya muda kidogo ilibidi Polisi waingilie kati kumuokoa.
Video ya tukio lenyewe hii hap
a

No comments:

Post a Comment