Wednesday, November 18, 2015

DIAMOND  PLATNUMZ NA PATRICK NGOWI KWENYE LIST YA WAAFRIKA 10 MABALOZI WA TUZO ZA #TFAA2015


Najua ukianza kutaja list ya Tuzo ambazo mastaa wengi wamekuwa wakiingizwa kushiriki na kushindania, huenda jina la Tuzo za TFAA sio jina ambalo umelisikia mara kwa mara.
The Future Awards Africa (TFAA) ni Tuzo ambazo hutolewa kila mwaka kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-31 waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka husika, Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2004 na vijana wa Nigeria na mwaka 2015 zinatimiza miaka 10 ambapo kwenye list ya vijana waliotajwa kama Mabalozi waliowahi kushinda Tuzo hizo kwenye kipindi cha miaka 10, majina ya Watanzania wawili nayo yamo, Naseeb Abdula.k.a Diamond Platnumz na Patrick Ngowi.

Dimdond
Diamond Platnumz.
PATRICK
Patrick Ngowi.
 List ya Mabalozi wote 10 waliowataja hii hapa
Bukola ‘Asa’ Elemide – Msanii wa muziki toka Nigeria
Michel ‘Don Jazzy’ Ajere – Producer wa muziki na msanii pia kutoka Nigeria
Tara Fela Durotoye – Mrembo kutoka Nigeria
Ndindi Nwuneli – Mwanzilishi wa Taasisi ya LEAP Africa iliyopo Nigeria
Nnaemeka Ikeguonu – Mjasiriamali wa masuala ya Kilimo Nigeria
Sangu Delle – Mwanaharakati kutoka Ghana
Patrick Ngowi – Mjasiriamali wa masuala ya nishati ya umeme wa jua kutoka Tanzania
Diamond Platinumz – msanii wa muziki kutoka Tanzania 
Fogblanbenchi Lily Haritu – Mwanaharakati kutoka Cameroon
Oramait Alengoil – Mbunge kutoka Uganda
Kama unahitaji kuifahamu zaidi TFAA Awards unaweza kuingia hapa mtu wangu >>> TFA
A

No comments:

Post a Comment