Papa awataka Wakristo wasilipize kisasi
Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya Wakristo na Waislamu.
Papa
Francis alikutana na Waislamu waliokwama katika sehemu ya mji
unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa kikristo
waliojihami vikali wa Anti-Balaka.
Asili mia kubwa ya takriban
waislamu laki moja nchini humo, walikimbia mji huo kufuatia mapigano
yaliyodumu kwa ziaidi ya miaka mitati.
Misikiti mingi iliharibiwa wakati wa vita hivyo.
Papa Francis amewataka wasameheane na waache kulipiza kisasi.
''Wakristo na Waislamu ni ndugu ,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
''hatupaswi kulipiza kisasi na kumdhuru mtu yeyote kwa jina la mungu'' alisema Papa Francis.
Hivi
sasa leo Papa Francis anaongoza misa yake ya mwisho barani Afrika
katika uwanja mkuu wa kitaifa ambako anatarajiwa kutoa wito wa
maridhiano, amani na utengamano.
No comments:
Post a Comment