Wengi wauawa mashambulio Paris
Ufaransa
imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya
120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu
wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo
wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na
Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.
Shambulio
mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema
watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa
baada ya kushikwa mateka.
Akiongea baada ya kufika katika ukumbi
huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika
watakabiliwa "bila huruma".
Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya
Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako
mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa
wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki
Mtu
aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi
zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika
mtaa nambari 11.
Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.
Rais
wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio
lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia
Ufaransa kukabiliana na waliohusika.
"Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.
"Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.”
Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio
hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia.
No comments:
Post a Comment