Visa vipya vya ebola vyatangazwa Liberia
Maafisa wa afya wa
Umoja wa Mataifa wanasema kumetokea maambukizi mapya ya Ebola nchini
Liberia chini ya miezi mitatu baada ya nchi hiyo kutangazwa kutokuwa na
ugonjwa huo.
Mgonjwa wa sasa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kumi kutoka viungani mwa mji wa, Monrovia.
Wachambuzi
wanasema habari hii ni pigo kubwa kwa nchi ya Liberia ambayo
imeshuhudia zaidi ya maambukizi elfu kumi na vifo zaidi ya elfu nne
tangu ugonjwa wa Ebola kugunduliwa nchini humo.
No comments:
Post a Comment