Gambia yapiga marufuku tohara ya wanawake
Rais wa Gambia,
Yahya Jammeh,amepiga marufuku tohara ya wanawake nchini humo akisema
inakwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.
Umoja wa mataifa unasema karibu robo tatu za wanawake wa Gambia wamefanyiwa ukeketaji.
Watabibu
wamekuwa wakieleza matatizo ya kiafya yanayotokea kutokana na tabia
hiyo lakini hilo halijapunguza visa vya upashaji tohara wanawake nchini
hiumo.
Sasa rais Yahya Jameh amesema amekuwa akitafiti kwa
muda wa miaka 21 katika kitabu tukufu cha Quran na vilevile kupitia
mahojiano na wanazuoni wa kiislamu na hamna ushahidi wowote wa
kufungamanisha kitendo hicho na dini ya Kiislamu.
No comments:
Post a Comment