Haya ndio maamuzi mapya ya mahakama kuhusu katibu mkuu wa zamani wa Simba….
Aliyekuwa katibu mkuu wa Simba na mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Pwani (COREFA) Hassanoo jina lake limeingia katika headlines November 13 baada ya mahakama kufanya maamuzi mapya, katibu mkuu huyo wa zamani wa Simba alikaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili ila November 13 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana.
Awali Hassanoo
aliwekwa ndani kwa kutuhumiwa kwa makosa matatu yakiwemo kosa la
kuhujumu uchumi kwa kusafirisha pembe za ndovu zinazotajwa kuwa na
thamani ya Tsh bilioni 1.1 kutoka Tanzania kwenda Hong Kong China. Hata hivyo katibu mkuu huyo wa zamani wa Simba anakabiliwa na kosa la wizi wa tani 26.475 za shaba kutoka Zambia zinazotajwa kuwa zaidi ya Tsh milioni 300 za kibongo.
Kosa hilo linatajwa kuwa kinyume na kifungu 258, 265 na 269 (C) vya kanuni ya dhahabu ya mali ya Kampuni ya Liberty Express Tanzania Ltd shitaka ambalo lilifunguliwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa serikali DPP. Hata hivyo Hassanoo yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza vigezo.
No comments:
Post a Comment