Kipigo cha Ethiopia chawarejesha Kilimanjaro Stars Tanzania, Full Time ya CECAFA Nov 30
Michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup
yameendelea leo November 30 kwa kupigwa mechi za kwanza za robo fainali
ya michuano hiyo, miongoni mwa mechi za robo fainali zilizochezwa leo
November 30 ni mechi kati ya timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ilicheza dhidi ya mwenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ethiopia.
Hii ni mechi ya robo fainali iliyokuwa
inazikutanisha timu zilizokuwa kundi moja na mchezo wao wa mwisho
walicheza na kumaliza kwa sare ya goli 1-1, November 30 Kilimanjaro Stars ilicheza mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili lakini kilikuwa na mabadiliko kidogo. Mchezo huo ambao Kilimanjaro Stars walianza kwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa nahodha wao John Bocco dakika ya 24, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya goli 1-1 baada ya Panom Cathuoch kuisawazishia goli Ethiopia dakika 57.
Kwa kawaida ya michuano hiyo kwa mechi
za robo fainali umaliziwa kwa mikwaju ya penati kama dakika 90
zitamalizika kwa sare yaani bila kupata mshindi, hapo ndipo Kilimanjaro Stars ilikosa bahati na Ethiopia kufuzu hatua inayofuata kwa kwa kufanikiwa kushinda jumla ya penati 4-3.
No comments:
Post a Comment