Monday, November 16, 2015

Paris: Mshukiwa mkuu ni raia wa Ubelgiji

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Paris ni raia wa Ubelgiji
Uchunguzi unaofanywa kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi mjini Paris unaonekana kumulika raia mmoja wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco anayedhaniwa kuwa ndiye aliyepanga njama hiyo.
Abdelhamid Abaaoud - mwenye umri wa miaka 20- aliishi katika eneo moja na washambuliaji wawili.
Maafisa wa usalama wanaamini kuwa sasa yuko nchini Syria ambapo anashirikiana na wanamgambo wa Islamic State.
Maafisa wa Usalama wa Ufaransa wamewatambua washambuliaji wengine wawili.
Samy Amimour anaaminika kuwa mmoja wa washambuliaji waliojitoa mhanga katika ukumbi wa sanaa.
 
Samy Amimour anaaminika kuwa mmoja wa washambuliaji waliojitoa mhanga katika ukumbi wa sanaa.
Mshambuliaji mwingine kwa jina Ahmad Al Mohammad,alijilipua katika eneo lingine.
Wakati huohuo Maafisa wamefanya uvamizi katika maeneo 168 nchini humo .
Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amesema watu 24 wamekamatwa na silaha kadhaa kunaswa.
Serikali ya Ufaransa inawahoji washirika wa vuguvugu moja la kijihadi ambao wanashukiwa kuwa ndio walioendesha mauaji ya zaidi ya watu 125 ijumaa usiku.
Waziri wa mambo ya ndani amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Polisi wanamsaka Salah Abdeslam, raia wa Mfaransa aliyezaliwa mjini Brussels.
Wachunguzi wanaamini mashambulio hayo yalipangwa na kundi moja nchini Ubelgiji kwa ushirikiani na watu waliokuwa ndani ya Ufaransa.
Kwa sasa maafisa wa polisi wanamsaka Salah Abdeslam, raia wa Mfaransa aliyezaliwa mjini Brussels.
Polisi nchini Ubelgiji wamevamia makao yake lakini hawakupata chechote katika kitongoji cha Molenbeek .
Kakake Mohammed, ni mmoja kati ya watu 5 walioachiliwa huru bila mashtaka yeyote na mahakama ya Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment