Obama kuisadia Ufaransa kuwaadhibu IS
Viongozi wa mataifa
20 yenye uchumi mkubwa zaidi duniani wanakutana huko Uturuki ambako
ajenda ya vipi kukabiliana na vitendo vya ugaidi vinatarajiwa kutawala
mazungumzo yao.
Mengi ya mataifa yanayoshiriki kikao hicho yamewahi kukumbwa na mashambulio kama hayo.Rais wa Uturuki Tayip Erdogan, anatarajiwa pia kuhimiza hatua za kumaliza vita vya Syria.
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa wanaandaa mikakati ya kujibu mashambaulizi ya alyopangwa na Islamic State mjini Paris Ufaransa.
Obama ameahidi kushirikiana na mwenzake wa Ufaransa kuwaadhibu wale waliotekeleza mauaji ya watu 129 ijumaa usiku.
Aidha viongozi hao wa mataifa yenye nguvu zaidi ulimwenguni wanakabiliwa na swali la iwapo waongeze mashambulio dhidi ya IS huko Syria au wabadili mkondo wa vipi kukabiliana vitendo vya kundi hilo.
Duru za White House zasema rais Obama anatarajiwa kuwa na kikao na mfalme wa Salman wa Saudia hapo kesho kama njia mojawapo ya kutafuta suluhu kwa mzozo wa Syria.
Wakati huohuo mashirika 20 na mataifa yakiwemo Urusi na Marekani wanasema - makubaliano yameafikiwa ya ratiba iliyopangwa kujaribu kumaliza vita vya Syria.
Mpango huo uliafikiwa baada ya mkutano mjini Vienna Austria
Mpango ni kuwa majadiliano baina ya serikali ya rais Bashar al Assad na makundi ya upinzani yaanze Januari kwa lengo la kuunda serikali ya mpwito kwenye kipindi cha miezi 6 ukifuatiwa na uchaguzi katika muda wa miezi 18.
Hatua hiyo inatakawa iandamane na hatua ya kusitisha mapigano itakayosimamiwa na umoja wa mataifa.
Hata hivyo bado hamna mwafaka mahsusi kuhusu mstakabali wa baadaye wa rais , Bashar al-Assad.
No comments:
Post a Comment