Ndege za Misri zapigwa marufuku Urusi
Mamlaka ya safari
za ndege nchini Urusi imepiga marufuku ndege za shirika la taifa la
ndege la Misri kuhudumu Urusi, msemaji wa uwanja wa ndege Moscow
amesema.
Safari za ndege kutoka Urusi hadi Misri tayari zilikuwa
zimesimamishwa baada ya ndege ya Urusi kuanguka eneo la Sinai mwezi
jana.
Abiria wote 224 walifariki, wengi wao wakiwa raia wa Urusi.
Shirika hilo la Egypt Air ndilo pekee lililokuwa limesalia likifanya safari kati ya mataifa hayo mawili.
Kundi
la Sinai Province, lenye ushirika na Islamic State, limedai kuhusika
katika kuangusha ndege ya Metrojet nambari 9268, iliyokuwa ikitoka Sharm
el-Sheikh kuelekea St Petersburg Urusi.
Mataifa ya Magharibi
yamesema kuna uwezekano mkubwa bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo ikiwa
angani, lakini Urusi na Misri zimesema ni mapema mno kuthibitisha hayo.
Baada ya ajali hiyo, mataifa kadha, ikiwemo Uingereza, yalisitisha
safari za ndege za kuingia na kutoka Sharm el-Sheikh, yakitaja wasiwasi
kuhusu usalama.
No comments:
Post a Comment