Papa 'wakristu wasilipize kisasi' Afrika ya Kati
Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui.
Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu.Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa Anti-Balaka.
Asili mia kubwa ya takriban waislamu laki moja nchini humo, walikimbia mji huo kufuatia mapigano yaliyodumu kwa ziaidi ya miaka mitati.
Misikiti mingi iliharibiwa wakati wa vita hivyo.
Papa Francis amewataka wasameheane na waache kulipiza kisasi.
''Wakristo na Waislamu ni ndugu ,hakuna faida yeyote inayotokana na uhasama''alisema papa.
''hatupaswi kulipiza kisasi na kumdhuru mtu yeyote kwa jina la mungu'' alisema Papa Francis.
Hivi sasa leo Papa Francis anaongoza misa yake ya mwisho barani Afrika katika uwanja mkuu wa kitaifa ambako anatarajiwa kutoa wito wa maridhiano, amani na utengamano.
No comments:
Post a Comment