Maduka ya dawa jirani na hospitali yanafungwa!! kingine kilichonifikia kutoka Wizara ya afya ni hiki…
Jana katibu mkuu wa Wizara ya afya Dk.Donan Mmbando
alizungumzia kuhusu mikakati ya kutaka kufunga maduka ya dawa yaliyo
karibu na hospitali za Serikali kwa madai ya malalamiko ya wizi wa dawa
hizo kutoka hospitali.
Leo Msemaji wa Wizara hiyo Nsachris Mwamwaja amezungumzia
moja ya mikakati ya Wizara hiyo ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na
maduka ya dawa ndani ya hospitali ambayo yatakuwa ya Serikali chini ya
Bohari kuu ya dawa MSD.
“Hospitali ya Muhimbili ina maduka ya
dawa ndani, tumepanga kuhakikisha kila hospitali ya Serikali inakuwa na
duka ndani, na tutahakikisha dawa zote zitakuwepo, lengo ni kuondoa
malalamiko ya watu kuwa yale maduka ndio chanzo cha kukosekana kwa dawa
mahospitalini”...Nsachris Mwamwaja
“Ni kweli haya maduka yapo sehemu
ambazo wauguzi ndio hutoa maelezo wagonjwa wakanunue hizo dawa katika
maduka hayo, wagonjwa wanaotumia huduma za mifuko ya jamii pia watakuwa
wakitumia maduka ya hospitali za Seeikali, nia yetu ni wagonjwa wapate
dawa bila usumbufu wowote”..
Kingine kilichosikika kutoka ndani ya Wizara hiyo ni utapeli ambao
umekuwa ukifanywa kwa waajiri ambapo kumejitokeza wimbi la matapeli na
kuwapangia watu maeneo ya kwenda kufanya kazi kitu ambacho si kweli kwa
kuwa Wizara hiyo haijatoa majina ya ajira na haijawapangia watu vituo
vya afya.
“Kuna taratibu za kukufanya uingizwe
kwenye mfumo wa kulipwa na Wizara, ni ngumu kuingia kirahisi huo ni
udanyangifu unaofanywa na baadhi ya watu ambao si waaminifu katika
baadhi ya ofisi..pia wizara haitoa barua wala kuajiri bali inatoa majina
na kupeleka kwa waajiri husika”…
No comments:
Post a Comment