Mambo matano mapya ya kufahamu kuhusu ujenzi wa barabara za juu Dar es salaam
Kwenye moja ya ahadi za Dr. John Pombe Magufuli
wakati akiwa kwenye kampeni ya kugombea Urais wa kuiongoza Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania, ilikua ni kujenga barabara za juu kwenye jiji la Dar es salaam ili kusaidia kupunguza foleni.
Rais Magufuli aliingia kwenye headlines za moto
ndani ya saa 24 tu baada ya kuapishwa kwa kuanza kufanya ziara za
kushtukiza kwenye taasisi za serikali kama Wizara ya fedha pamoja na
hospitali ya taifa Muhimbili akionyesha kwamba kazi ndio imeanza, na
sasa anazimiliki headlines kwenye barabara za juu.
Yafuatayo ni mambo matano ambayo yatakupa uhakika kwamba barabara za
juu Dar es salaam zinanukia na mradi wake umeanza kufanyiwa kazi, ungana
na Mkurugenzi mkuu wa TANESCO Injinia Felchesmi Mramba kwenye kauli zake baada ya TANESCO kuambiwa isogeze mitambo yake kupisha ujenzi wa hizo barabara.
1 – ‘Ni kweli ipo kazi kubwa inayofanywa na serikali kupanua barabara na kuweka barabara za juu katika maeneo mawili ambayo ni TAZARA na Ubungo.
2 – Kwenye maeneo yote mawili miundombinu ya umeme ya TANESCO ipo na hasa eneo la Ubungo ambako kuna laini kubwa, kwa TAZARA tayari tulishahamisha laini zetu na kupisha eneo la upanuzi wa hizo barabara za juu na sasa zinaweza kujengwa bila tatizo.
3 – Kwa Ubungo kuna kazi kubwa zaidi kuliko TAZARA
kwa sababu ya kuhamisha laini kubwa ya KV 132, kazi ya kuihamisha
itaanza mwezi wa kwanza mwaka 2016 na itaweza kuchukua miezi kama mitatu
mpaka sisi kumaliza kuiondoa.
4 – Laini kubwa inayotoa umeme kutoka Ubungo kwenda kituo kikubwa cha katikati mjini cha Ilala ndio inayotakiwa kunyanyuliwa juu sana kwahiyo tutajenga minara mipya mirefu zaidi ambayo itakwenda juu zaidi.
5 – Kazi ya TAZARA imefanywa na Mainjinia wa Kitanzania ila hii ya Ubungo ambayo ni kazi kubwa itafanywa na Mainjinia wa Kijapan.
No comments:
Post a Comment