EU, Uturuki zakubaliana suala wakimbizi
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Umoja wa ulaya na
uturuki wafikia makubaliano ya jinsi ya kuchukua hatua ili kuondokana na
mafuriko ya wakimbizi na wahamiaji ndani ya bara la Ulaya, mkutano huo
umefanyika nchini Ubeljiji katika makao maku ya EU.
Chini ya
makubaliano hayodolla bilioni 3 zitatolewa na Umoja huo(EU) ili kusaidia
wakimbizi kutoka nchi ya Syria wanaoelekea Uturuki.
Tayari Ankara imeshatumia dolla billioni 8 kutatua matatizo mbali mbali ya wageni hao.
Mazungumzo hayo yali fufua pia mjadala ju ya Uturuki kujiunga katika
nchi zenye kuunda Umoja wa Ulaya na likazungumzwa pia la nchi hiyo
kusafiri bila mipaka ndani ya bara hilo katika maeneo yaliyokubaliwa
kutumia visa moja iitwayo shcenghen.
Waziri mku wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema ni tukio la kihistoria katika mahusiano ya ututruki na Umoja wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment