Ufaransa yachunguza mkanda wa kujilipua
Polisi wa Ufaransa wanatathmini kile kinachoaminika kuwa ni mkanda wa kujitoa muhanga, uliopatikana kusini mwa mji wa Paris
Watu wanaokusanya taka ndio waliokiona kitu hicho katika pipa la taka huko Montrouge.
Vyanzo
vya polisi vinasema, kitu hicho kinafanana na mikanda iliyotumika
katika mashambulio ya mjini Paris, ambayo ina sehemu ya mbele na ya
nyuma ya kuwekea chaji.
Pia inachunguzwa ili kubaini iwapo mkanda huo ulivaliwa na mshukiwa mkuu Salah Abdeslam.
Wakati
huo huo, kwa mara ya kwanza Ufaransa, imepeleka vikosi vyake kupambana
na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu IS kupitia meli yake ya kubeba
ndege za kijeshi ya Charles de Gaulle.
No comments:
Post a Comment