Mtoto aliyeugua Ebola apona Guinea
Maafisa wa afya
nchini Guinea wamesema mgonjwa wa mwisho aliyeripotiwa kupata maradhi ya
Ebola amepona na ameruhusiwa kutoka kwenye kituo cha matibabu mji mkuu
wa nchi hiyo, Conakry.
Ugonjwa huo ulioanza nchini Guinea, umeua
zaidi ya watu 11,000 Afrika magharibi.Nchi jirani Sierra Leone na
Liberia zilifanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa Ebola.
Mgonjwa mmoja
aliyekuwa amebaki ni mtoto wa siku 19 ambaye mama yake alifariki
kutokana na ugonjwa huo.msemaji wa kitengo kinachoratibu mapambano dhidi
ya Ebola amesema vipimo vilivyochukuliwa mara mbili vimethibitisha kuwa
mtoto huyo amepona.
Mwishoni mwa juma lililopita, kundi la watu takriban 70 waliokuwa wamewekwa karantini waliruhusiwa.
Lakini
maendeleo haya chanya hayamaanishi kuwa Guinea imefanikiwa, ili kufikia
hatua hiyo inapaswa kusiwe na mgonjwa mpya kwa kipindi cha wiki sita
zijazo.
No comments:
Post a Comment