Urusi kushirikiana kupambana na IS
Urusi imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.
Rais
Vladmir Putin amemwambia mweziye wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa
shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini
Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya
nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo.
Rais huyo wa Ufaransa
yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza
kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini Syria.
No comments:
Post a Comment